Posts

Showing posts from June, 2022

YANGA YATOA TAMKO ZITO CAF, WATAKA KUWEKA HISTORIA MPYA

Image
  KUELEKEA mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, uongozi wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Yanga umechimba mkwara mzito kwa kusema tayari umeanza kufanya maandalizi mazito ya ndani na nje ya uwanja kuhakikisha wanaandika rekodi ya kufika mbali katika michuano hiyo. Yanga tayari imekata tiketi ya uwakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanikiwa kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu, huku wakiandika rekodi ya kushinda ubingwa huo mara 28. Katika michuano hiyo msimu uliopita Yanga waliondolewa katika hatua ya awali, mara baada ya kukubali kipigo cha jumla cha mabao 2-0 kutoka kwa Rivers United ya Nigeria, ambapo walifungwa bao moja nyumbani na moja ugenini. Akizungumza na Championi Jumatano, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Injinia Hersi Said alisema: “Tunafahamu kuwa mashindano ya kimataifa sio jambo dogo, ni wazi kuwa tunapaswa kufanya kazi kubwa ili kupata mafanikio katika mashindano hayo kwa kuwa ...

LIGI IMEFIKA UKINGONI,HIZI HAPA ZIMESHUKA,YANGA REKODI

Image
  MSIMU wa 2021/22 umekamilika ambapo mbivu na mbichi zimejulikana. Biashara United ya Mara itacheza Champioship msimu ujao ikiungana na Mbeya Kwanza ya Mbeya. Mtibwa Sugar wao watacheza mtoano na Tanzania Prisons ili kusaka timu itakayobaki ndani ya ligi. Matokeo yapo namna hii:-  Kagera 0-0 Polisi Tanzania. Mbeya Kwanza 0-0 Simba, Yanga 1-0 Mtibwa  mtupiaji ni Dennis Nkane dk  ya 80 Dodoma Jiji 1-0 KMC mtupiaji ni Wazir Jr dk12. Ruvu Shooting 1-0 Tanzania Prisons, Fullu Maganga dk 10 Coastal Union 1-1 Geita Gold Chambo  dk 20 kwa Coastal Union na George  Mpole dk10. Mbeya City 1-1 Namungo ni Ssemujju alitupia dk ya 47’ kwa Mbeya City,Sixtus Sabilo dk 17. Azam 4-1 Biashara  ni mabao ya Mbombo dk 13 kwa mkwaju wa p, dk 46, dk 64 na  Tigere 79 huku lile la Biashara likifungwa na  Kabeja 72.

EXCLUSIVE: DEREVA ALIYEENDESHA BASI LA YANGA LA UBINGWA KUTOKA UGANDA, AFUNGUKA MENGI USIYOYAJUA..

Image
  GLOBAL TV imefanya mahojiano na Dereva aliyeendesha gari walilotumia Yanga kwenye kushangilia Ubingwa wao jana juni 26, ambalo limetoka nchini Uganda.

YANGA Wafunga BARABARA, MSAFARA Wao HAUJAWAHI KUTOKEA, ANAIMBWA GSM tu HUKO, AZIZ KI Atajwa!

Image

WAKATI MWINGINE KUPIGA HESABU KIMATAIFA

Image
WAKATI mwingine tena wa kukamilisha hesabu kwenye mipango ya kimataifa hasa kwa timu ambazo zinakibarua cha kufanya hivyo kimataifa. Haikuwa kazi ngumu kwa msimu uliopita kwa timu za Tanzania kuweza kupeta kimataifa kwa kuwa kila timu ilikuwa inakwenda kwa mwendo wake wa kusuasua. Azam FC licha ya kuwa imara kwenye miundombinu pamoja na wachezaji wazuri bado kimataifa walishindwa kututuoa kimasomaso Watanzania. Kwa upande wa Yanga nao pia walikwama kufika hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku wale waliokuwa wanapewa nafasi ya kufanya vizuri kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho. Simba ambao walitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu walifungashiwa virago mapema kwenye Ligi ya Mabingwa na kuangukia Kombe la Shirikisho. Kwa yote ambayo wamefanya licha ya kuishia hatua ya robo fainali bado tulishindwa kuwa na wawakilishi kwenye Ligi ya Mabingwa. Muda huu ambao upo hasa ligi ikifika ukingoni ni wakati sahihi wa kuweza kuanza kuweka mipango upya kwa ajil...

YANGA SC YAENDELEZA REKOD YA KUTOPOTEZA MECHI LIGI KUU

Image
MABINGWA, Yanga wameendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.   Mshambuliaji Mkongo, Heritier Makambo alianza kuifungia Yanga dakika ya 40, kabla ya kiungo Mganda, Joseph Ssemunju kuisawazishia Mbeya City kwa penalti dakika ya 50 kufuatia Nahodha, Bakari Mwamnyeto kuunawa mpira kwenye boksi. Yanga wanafikisha mechi 29 bila kupoteza mechi, wakiwa tayari mabingwa kwa pointi zao 71, nyuma yao wakiwa mabingwa wa misimu minne iliyopita, Simba SC wenye pointi 60 za mechi 28 na kesho watamenyana na Tanzania Prisons hapo hapo Sokoine, Mbeya. Kwa Mbeya City, sare hiyo inawafanya wafikishe pointi 39 baada ya mechi 29 katika nafasi ya tisa. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union bao pekee la beki David Luhende dakika ya 15 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Nayo imeichapa Polisi T...

FT:MBEYA CITY 1-1 YANGA, UWANJA WA SOKOINE

Image
MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga umekamilika Uwanja wa Sokoine kwa timu zote mbili kugawana pointi mojamoja. Ni Yanga walianza kupata bao la kuongoza kwenye mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkuwa mwanzo mwisho. Bao la Heritier Makambo ilikuwa dk ya 39 liliweza kujazwa kimiani na lilidumu mpaka dk ya 49 kipindi cha pili. Kwa Mbeya City ni bao la Ssemuja Joseph aliweza kupachika bao hilo dk ya 49 kwenye mchezo ambao mabingwa wa ligi Yanga watakaidhiwa ubingwa wa ligi.

KOMBE LIPO UWANJA WA SOKOINE,MBEYA CITY 0-1 YANGA

Image
 KOMBE Jipya la Ligi Kuu Bara la NBC lipo Uwanja wa Sokoine, Mbeya,ambapo mabingwa wa msimu wa 2021/22 watakabidhiwa mara baada ya kukamilisha dk 90 mbele ya Mbeya City. Kwa sasa mchezo ni mapumziko ampabo ubao unasoma Mbeya City 0-1 Yanga mtupiaji akiwa ni Heritier Makambo dk ya 39 kwa shuti lililoweza kugonga mwaba kabla ya kusindikizwa na beki wa Mbeya City. Mbeya City watakamilisha dk 90 wakiwa pungufu kwa saabu nahodha wao Mpoki Mwakinyuke ameonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Ilikuwa ni dk ya 43 baada ya kuweza kumchezea faulo beki Djuma Shaban wa Yanga.

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MBEYA CITY

Image
 HIKI hapa kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City,Uwanja wa Sokoine Mbeya hiki hapa:- Diarra Djuma Yassin Mwamnyeto Job Bangala Aucho Sure Boy Ushind Makambo

WAPE TABASAMU KUFANYIKA UWANJA WA SABASABA,MORO

Image
ANAANDIKA Dickson Job,beki wa kikosi cha Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Starsnamna hii:-Habari watanzania. Mimi ni DICKSON JOB mchezaji wa Klabu ya Yanga. Nawakaribisha kutuunga mkono Katika siku maalumu tuliyoiandaa kwaajili ya kutoa Shukran zetu kwa jamii tuliyoipa jina la WAPE TABASAMU itakayofanyika tarehe 08/07/2022 Mkoani Morogoro. Siku hii ni maalumu kwaajili ya kuwafariji watoto yatima wanaoishi Katika vituo mbalimbali mkoani MOROGORO pamoja na kutoa msaada kidogo kwa wamama wajawazito wanaohudumiwa katika Hospitali ya mkoa Morogoro. Pia kutakuwa na mchezo wa hisani Kati ya TEAM JOB vs TEAM KIBWANA utakaokuwa ni mahususi kwa kuchangisha fedha kwaajili ya mahitaji ya watoto hao. Mchezo huu utafanyika katika Uwanja wa Sabasaba,Moro kwa kiingilio cha sh 1,000 tu. Tunawakaribisha wote watakaoguswa kuungana na sisi kwa chochote kile watakachobarikiwa. Namba: 0716678781 Jina: Seif Hamisi WAPE TABASAMU WAFARIJIKE.

HAJI MANARA: FEI TOTO HATUWEZI KUMUUZA CHINI YA BILIONI 1

Image
“Mchezaji kama Feisal sasa hivi anamkataba, inakuja Klabu labda kutoka South Afrika inakuletea ofa ya USD 50,000 au USD 100,000 hatuwezi kukaa kuzungumza naye huyu mtu. “Hapa katikati zimekuja ofa za baadhi ya timu, hatuwezi kumuuza Feisal Chini ya Tsh. Bilioni 1 sawa na Kama USD 500,000 hapo angalau tunaweza kuzungumza,” Msemaji wa Yanga, Haji Manara

YANGA WATUMIA GARI LA MADRID KUBEBEA KOMBE

Image
YANGA SC wanataka kuzifundisha timu nyingine namna gani ya kushangilia ubingwa msimu huu, hiyo ni baada ya Msemaji wa Yanga, Haji Manara kuweka wazi kwamba wameagiza gari maalumu la kubeba wachezaji na kutembeza kombe lao. Manara anasema, basi ambalo wameagiza ni kama lile walilolitumia Real Madrid kushangilia ubingwa wao wa La Liga na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2021/22. Yanga tayari wameshatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na wanatarajiwa kukabidhiwa kombe hilo Jumamosi hii katika mchezo dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Akizungumza jinsi ambavyo Yanga watalitembeza kombe lao, Manara alisema: “Lazima tuwafundishe timu nyingine jinsi gani ya kuushangilia ubingwa wa ligi kuu. “Tayari tumeshaagiza gari maalumu kwa ajili ya kuushangilia ubingwa huo, gari hilo linafanana na ambalo walilitumia Real Madrid na Liverpool kushangilia makombe ambayo waliyabeba msimu huu. “Kuhusu utaratibu, mashabiki wote wa Yanga Jumapili tunawakaribisha uwanja wa ndege k...