BEKI WA MABINGWA ATUA SINGIDA BIG STARS

 

BEKI wa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho msimu wa 2021/22 ametua ndani ya kikosi cha Singida Big Stars.

Yanga jana Julai 2 iliweza kukamilisha msimu kwa kutwaa Kombe la Shirikisho kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Coastal Union kwa ushindi wa penalti 4-1 baada ya dk 120 kukamilika kwa kufungana mabao 3-3,Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Taarifa kutoka Singida Big Stars imeweka wazi kuwa:”Tumefanikiwa kuinasa saini ya beki no 2 kutoka kwa mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania Yanga. Godfrey amesaini mkataba wa miaka 2 kuitumikia timu yetu,”.

Nyota huyo kwa msimu wa 2021/22 hakuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nai kutokana na uwepo wa Djuma Shaban ambaye alikuwa chaguo la kwanza.

Comments

Popular posts from this blog

HAJI MANARA AMPONGEZA ALLY KAMWE KUTEULIWA YANGA

AZAM FC YASHINDA 2-0 CHAMAZI, LAKINI YATOLEWA

WAWAKILISHI WA KIMATAIFA YANGA KUREJEA DAR