KIUNGO WA KIMATAIFA KUTAMBULISHWA YANGA

 

KIUNGO Aziz KI  anatarajiwa kutambulishwa leo Julai 14 na mabosi wa Yanga baada ya kusaini dili la miaka miwili.

Nyota huyo alikuwa anacheza ASEC Mimosas mkataba wake umegota ukingoni hivyo atajiunga na Yanga akiwa ni mchezaji huru.

Anakwenda kuungana na kiungo Bernard Morrison ambaye aliwahi kucheza naye kwenye mashindano ya kimataifa zama zile Morrison alipokuwa ndani ya Simba.

Tayari kwa sasa Morrison naye pia ametambulishwa ndani ya Yanga akiwa ni mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake ndani ya Simba.

Taarifa zimeeleza kuwa Aziz KI yupo Bongo kwa muda kwa ajili ya kukamilisha dili hilo ambalo limekamilika kwa asilimia kubwa na kilichobaki ni kutamulishwa

Comments

Popular posts from this blog

HAJI MANARA AMPONGEZA ALLY KAMWE KUTEULIWA YANGA

AZAM FC YASHINDA 2-0 CHAMAZI, LAKINI YATOLEWA

WAWAKILISHI WA KIMATAIFA YANGA KUREJEA DAR