Kocha Mkuu wa YANGA Sc Naseerdeen Nabi (Professa) ameshinda Tuzo ya kuwa Kocha Bora katika ligi ya NBC msimu wa 2021-2022, Tuzo zilizotolewa hapo jana tareh 7 July.
ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa baada ya kutangazwa rasmi kwenye Idara ya Habari na Mawasiliano alipongezwa na Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Yanga. Ameweka wazi kuwa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba naye alimpa pongezi. Septemba 27, Kamwe alitangazwa kuwa Ofisa Habari na Priva Abiud maarufu kama Privaldinho alitangazwa kuwa Msimamizi Mkuu wa Digital na Maudhui. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na +255 Global Radio kwenye kipindi cha Krosi Dongo, jana Kamwe alisema kuwa alijisikia kuwa mwenye furaha baada ya kutangazwa kuanza majukumu mapya. “Baada ya kutangazwa nimepewa pongezi nyingi ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Haji Manara na Ahmed Ally, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba wote wamefurahi mimi kutangazwa. “Nilifurahi nilipopewa taarifa hizi kwa kuwa mimi ni shabiki wa Yanga na kazi kubwa ambayo nitafanya ni kushirikiana na wengine ili kufikia malengo yetu,” alisema Kamwe
WENYEJI, Azam FC wametupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Akhdar ya Libya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Idris Mbombo dakika ya 28 na Ededen Essien aliyejifunga dakika ya 59 na kwa matokeo hayo Al Akhdar inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mechi ya kwanza.
BAADA ya kupoteza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal, kikosi cha Yanga leo kimeanza safari ya kurejea Tanzania. Msafara huo ambao uliongozana na viongozi utapitia Addis Ababa Ethiopia. Bado Yanga inabaki kwenye anga za kimataifa kwa kuwa imeangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrka. Inafanya zibaki timu mbili Tanzania ambazo zinapeperusha bendera ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Simba. Azam FC na Kipanga wao jitihada zao ziligota mwisho baada ya kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zao ambazo walicheza. Azam licha ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Al Akhadar ya Libya imeondolewa kwa jumla ya mabao3-2 kwa kuwa mchezo wa ugenini ilipoteza huku Kipanga wenyewe wakiondolewa kwa jumla ya mabao 7-0 dhidi ya Club Aficain.
Comments
Post a Comment