Posts

Showing posts from September, 2022

SIMBA YA JUMA MGUNDA YAWEKA REKODI DK 180

Image
   NDANI ya dakika 180, Zanzibar, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda ameshuhudia wachezaji wake wakishinda mechi zote mbili. Kwenye mechi hizo Simba haijaruhusu bao la kufungwa huku ikifunga jumla ya mabao manne, moja ni kwa pigo la penalti. Mchezo wa kwanza ilikuwa dhidi ya Malindi FC ambapo Simba ilishinda bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni mzawa Nassoro Kapama aliyetumia pasi ya Peter Banda. Mchezo wa pili, Simba ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Kipanga kwenye mchezo uliochezwa jana, Septemba 28. Mabao ya Simba yalifungwa na Augustino Okra ambaye alitupia mabao mawili dakika ya 36 na 59 huku moja likifungwa na Kibu Dennis. Mchezo wa mwisho kwa Mzungu wa Simba, Dejan kucheza ilikuwa dhidi ya Malindi na hakuyeyusha dakika 90.

HAJI MANARA AMPONGEZA ALLY KAMWE KUTEULIWA YANGA

Image
  ALLY Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa baada ya kutangazwa rasmi kwenye Idara ya Habari na Mawasiliano alipongezwa na Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Yanga. Ameweka wazi kuwa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba naye alimpa pongezi. Septemba 27, Kamwe alitangazwa kuwa Ofisa Habari na Priva Abiud maarufu kama Privaldinho alitangazwa kuwa Msimamizi Mkuu wa Digital na Maudhui. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na +255 Global Radio kwenye kipindi cha Krosi Dongo, jana Kamwe alisema kuwa alijisikia kuwa mwenye furaha baada ya kutangazwa kuanza majukumu mapya. “Baada ya kutangazwa nimepewa pongezi nyingi ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Haji Manara na Ahmed Ally, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba wote wamefurahi mimi kutangazwa. “Nilifurahi nilipopewa taarifa hizi kwa kuwa mimi ni shabiki wa Yanga na kazi kubwa ambayo nitafanya ni kushirikiana na wengine ili kufikia malengo yetu,” alisema Kamwe

VIDEO: MANDONGA MTU KAZI AMVAA MWAKINYO

Image
BONDIA mwenye mbwembwe nyingi ulingoni Mandonga mtu kazi ameweka wazi kuwa anamtaka Hassan Mwakinyo kwenye pambano

HIZI HAPA SABABU 4 ZA MZUNGU "DEJAN" KUONDOKA SIMBA SC

Image
  DEJAN maarufu kama Mzungu wa Simba jana alitoa taarifa kuhusu kuvunjika kwa mkataba wake ndani ya kikosi cha Simba, hizi hapa sababu nne ambazo zimefanya nyota huyo kuondoka

MZEE WA KUCHETUA KARUDI, KUWAKOSA SIMBA

Image
  KIUNGO wa Yanga, Bernard Morrison amezidi kuwa imara hali yake na tayari ameanza mazoezi na wachezaji wenzake. Nyota huyo alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambao waligawana pointi mojamoja. Ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-2 Azam FC na Morrison aliyeyusha dakika 90 lakini alikuwa amepata maumivu. Licha ya kuanza mazoezi nyota huyo hatacheza mechi tatu zinazofuata kwenye ligi za Yanga baada ya kufungiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi iliyo chini ya Shirikisho la Mpira Tanzania, (TFF). Sababu ya nyota huyo mwenye bao moja ndani ya ligi ambalo aliwatungua Coastal Union Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni kile kilichoelezwa kuwa alimkanyanga kwa makusudi mchezaji wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda. Miongoni mwa mechi ambazo Morrison atazikosa msimu huu ni pamoja na ule dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 23, Uwanja wa Mkapa. Pia atawakosa Namungo na Ruvu Shooting kwenye mtiririko wa adhabu hiyo na amet...

UBABE UBABE TU MTWARA, KIDUKU, MANDONGA MTU KAZI KAZINI

Image
  MASAA machache yamesalia kutoka hivi sasa leo Jumamosi Septemba 24, 2022 mabondia Twaha Kiduku na Abdo Khaled raia wa Misri kupanda ulingoni kuwania mkanda wa UBO Intercontinental kutoka Mtwara Ubabe Ubabe linalotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda wa Sijaona mkoani Mtwara. Kiduku na Khaled wa wamepima uzito na tayari kwa pambano hilo la uzani wa Super Middle ambalo litachezwa kwa raundi 10 huku wa kazi wa mkoani hapa wakitarajia kushuhudia  kutoka kw mabondia hao. Licha ya kuwepo kwa mapambano ya utangulizi ila bondia Karim Mandonga  amekuwa gumzo kubwa kwa watu wa mjini hapa kutokana na  umaarufu wa bondia huyo kutoka Morogoro kufuatia mikwara anayowapiga mabondia wenzake licha  ya kupokea vichapo mara kwa mara. Kiduku amewahakikishia Watanzania kuwa yupo tayari kuwapa burudani ya ushindi kwenye pambano hilo wakati mpinzani wake akisema  kuwa atamaliza raundi kumi za pambano hilo kwa kuamini atamchapa mpinzani wake. Mbali ya Kiduku, bondia Karim M...

NABI ATAKA KROSI, KONA BAO, MGUNDA ATENGA DAKIKA 180

Image
  NABI ataka krosi,kona bao, Mgunda atenga dakika 180 Simba ndani a Championi Jumamosi

U 23 YATOSHANA NGUVU NA SUDAN KUSINI AZAM COMPLEX

Image
  KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 leo Septemba 23 kimelazimisha suluhu dhidi ya Timu ya Taifa ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON. Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo wageni Sudan Kusini walicheza kwa umakini wakitumia mbinu ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza. U 23 ilianza kwa kasi kuliandama lango la Sudan Kusini lakini umakini ulikosekana ndani ya dakika 15 za mwanzo kuweza kupata bao la kuongoza. Nahodha wa U 23, Kelvin John amesema kuwa walikuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo lakini imeshindikana hivyo benchi la ufundi litaona namna ya kuboresha. Kocha Mkuu wa U 23, Hemed Morocco amesema kuwa mapungufu ambayo wameyaona watayafanyia kazi kwenye mechi ya marudio. “Wachezaji walicheza kwa kujitoa lakini muunganiko na umakini kwenye kumalizia nafasi ulifanya tukashindwa kupata matokeo, makosa ambayo tumefanya tutafanyia kazi na mchezo ujao tuna imani tutapa matokeo,”. Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa nch...

MAYELE ATOA KAULI YA KIMATAIFA

Image
  MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele amesema yeye na wachezaji wenzake hawana presha kuhusu mchezo wa raundi ya pili ya mtoano dhidi ya Al Hilal ya Sudan Kaskazini. Mayele ametoa kauli hiyo kwa kujiamini akisema ni halali yao kuingia makundi katika michuano ya Kombe la Mabingwa Afrika kwani wana wachezaji wazuri na wanajiamini, hivyo hawana presha na mechi kubwa. “Kuhusu mechi dhidi ya Al Hilal, wachezaji hatuna presha kabisa. Yanga tuna wachezaji wakubwa waliozoea mechi zenye presha kama Bangala, Djuma, Morrison, Aziz Ki na wengine, tumezioe presha. “Mfano mimi mechi yangu kubwa ya kwanza ya kimataifa CAF nikiwa AS Vita nilicheza dhidi ya Kabylie ya Algeria na Raja Casablanca ya Morocco, ule uwanja ulijaa kabisa, kwa hiyo tumezoea ile presha. “Kwa hiyo tutajitahidi hapa kwetu tupate matokeo mazuri, na kule kwao tutakwenda kupambana tena ili tuingine makundi,” amesema Mayele. Ikumbukwe kuwa Yanga wametinga raundi ya pili ya mtoano baada ya kuitoa Zalan FC kwa jumla ya bao 9-0, am...

WINGA DEMBELE ASIMULIA ALIVYOPOTEZA MIAKA MITANO

Image
  WINGA wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Ufaransa Ousmane Dembele amefunguka juu ya maumivu aliyoyapitia katika miaka yake mitano ya awali akiwa na kikosi chake cha Barcelona. Dembele ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha Taifa cha Ufaransa kinachoshiriki michezo ya Uefa Nations amefunguka akidai kuwa miaka yake mitano ya awali akiwa na Barcelona ilipotea bure kwani alikuwa akiandamwa na majeruhi yaliyohusisha maumivu ya mara kwa mara ya misuli. “Kuanzia mwaka 2017-2021 nilipoteza muda wangu mwingi bure, nimepoteza miaka yangu mitano, ilinilazimu nifanye kazi zaidi ili niweze kucheza, niwe na afya na ili niweze kucheza kidogo kidogo. “Nilikuwa nikisumbuliwa na maumivu ya misuli ya mara kwa mara. Mkufunzi wangu alinisisitiza zaidi kuwa kama sitafanya mazoezi ya kutosha maumivu yangeweza kujirudia, nikiwa na Koeman nilianza kupata unafuu lakini nikiwa na Xavi hali ndiyo imeimarika zaidi. Nilivyokuja Barca nilikuwa mdogo sana, na kimsingi najiachia ndiyo lakini siyo sana kama wa...

YANGA WAIPIGIA HESABU AL HILAL

Image
  KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa wameona ubora wa wapinzani wao Al Hilal ya Sudan hivyo watafanya maandalizi mazuri kupata matokeo. Nabi amesema ameona ubora wa Al Hilal ambao ameuficha kwa kukataa kuuweka wazi kwa kuhofia wapinzani kushtuka, zaidi akipanga kukiimarisha zaidi kikosi chake ili kuhakikisha anapata ushindi nyumbani na ugenini. “Mimi ni kama mwanajeshi, muda wowote nipo tayari kwa ajili ya mapambano, hivyo kukutana na Al Hilal nilitarajia. “Hivyo kama kocha nimekuwa na utaratibu wa kuwafuatilia wapinzani wangu kwa kuziangalia video za michezo yao ya mwisho waliyocheza kwa ajili ya kuwajua zaidi. “Wapinzani wetu Al Hilal tayari nimewaona na kuwafahamu wachezaji hatari wa kuchungwa, mbinu na mfumo wanaoutumia, kikubwa ninaendelea kukinoa kikosi changu kitakachopata ushindi,” alisema Nabi. Yanga itaanzia nyumbani dhidi ya Al Hilal ambapo mechi ya kwanza inatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 8, kisha marudiano ni Sudan kati ya Oktoba 14 na 16, mwaka huu.

KOCHA MBRAZILI AIBUKIA SIMBA, MASTAA YANGA WAIAPIA AL HILAL

Image
  KOCHA Mbrazili aibukia Simba,mastaa Yanga waiapia Al Hilal ndani ya Championi Ijumaa

MECHI MBILI ZA KIRAFIKI SIMBA KUCHEZA ZANZIBAR

Image
  MECHI mbili za kirafiki watacheza wakiwa Zanzibar watanza na Kipanga, Septemba 25 na Septemba 28 watacheza dhidi ya Malindi. Mechi hizi za kirafiki ni kutokana na mwaliko ambao wameupata kutoka Shirikisho la Soka la Zanzibar, (ZFF). Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa mechi zote zitachezwa saa moja usiku na itakuwa ni maandalizi kwa ajili ya mechi zao za kimataifa. Simba inatarajiwa kucheza na Clube de Agosto kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika ya nchini Angola. “Tuna mechi mbili za kirafiki ambazo tutacheza tukiwa huko mchezo wa kwanza utakuwa Jumapili na baada ya siku mbili tutacheza mchezo mwingine Uwanja wa Amaan. “Baada ya michezo hiyo miwili timu itarejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Agosto,” amesema.

LIGI YA MATAIFA YA ULAYA INAENDELEA NA MERIADIANBET WAMEJIPANGA KUTOA PESA KWA AJILI YAKO

Image
  Baada ya Ligi nyingi kusimama sasa moto umehamia kwenye michezo ya kimataifa ya kirafiki. Mataifa ya Ulaya yatakuwa uwanjani kuhakikisha heshima ya nchi inasimama na mashabiki wanapata burudani ya soka safi,  Meridianbet hawajakusahau wanamtonyo wako.   Macho ya wapenzi wa soka hayatakuwa na ukungu usiku wa Alhamisi, wakati kijana wa Kifaransa Kylian Mbappe akiwa mstari wa mbele na wenzake kuhakikisha heshima ya taifa la Ufaransa inaendelea kuwekwa dhidi ya Austria.  Meridianbet watakuheshimisha wewe na mkeka wako, tazama odds za gemu hii hapa. Majira ya saa 21:45 Croatia watashuka dimbani kukipiga na Denmark, hapa heshima inatafutwa kule kuna Luke Modric na kule kuna Christian Eriksen. Una machaguo kibao ya kusuka jamvi lako hapa,  tazama meridianbet wamekuwekea odds bomba mechi hii. Huku mchezo mwingine utawakutanisha Poland dhidi ya Uholanzi, yaani ni hivi vita ni vita tu, Lewandowsk atakuwa na kibarua kingine mbele ya wachezaji wenzake De Jong na Memphis D...

LUSAJO NEMBO YA MABAO UWANJANI

Image
  NEMBO ya Relliats Lusajo ukifika Uwanja wa Mkapa utaiona juu ikiwa metulia, fahari kubwa kwa anachokifanya ni jambo la kujivunia kwa mzawa huyu. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 alianza kwa kasi ya namna hii kwenye kucheza na nyavu mwisho akagotea namba 10. Pia alikuwa ni namba moja kwenye kutengeneza mabao alitengeneza pasi 6 za mabao hakika miguu yake ina ushkaji na nyavu. Kwa msimu huu ni namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi akiwa ametupia mabao matano katika mechi tano mfululizo. Hajapoa kwenye mechi zote ambazo ameanza alikuwa anafunga na anatimiza majukumu yake bila kuogopa. Anastahili pongezi na kuongeza juhudi kutimiza malengo yake pamoja na malengo ya timu ili aweze kuvunja rekodi yake mwenyewe. Huyu hapa Lusajo anazungumzia kasi yake hiyo:”Kikubwa ni ushindi kwa ajili ya timu na inapata matokeo, ushindani ni mkubwa na sisi tunazidi kupambana,”. Kwenye mabao matano ambayo amefunga ni bao moja kafunga kwa mkwaju wa penalti mbele ya Coastal Union huku akiifunga Mtibwa Su...

WAZAWA SIMBA WANSTAHILI PONGEZI KWA WALICHOKIFANYA

Image
  WAZAWA wawili ambao kwa sasa wanakinoa kikosi cha Simba wote wameanza mwendo wao kwa kasi nzuri wanastahili pongezi na kuongza juhudi zaidi katika kutimiza majukumu yao. Kocha Mkuu, Juma Mgunda ameanza kibarua kwenye nyakati ngumu kwa kuwa timu ilikuwa bado haijaungana na muunganiko wake ulikuwa unatafutwa. Kuondoka kwa Zoran Maki na mikoba yake kuwa mikononi mwa Mgunda akishirikiana na Matola kuna jambo limeongezeka kwa wazawa hawa. Michezo mitatu ambayo wamecheza wameshinda mechi zote mbili za kimataifa na moja ile ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons. Mwendo wao walianza Big Bulets 0-2 Simba na Simba 2-0 Big Bullets kisha ule wa ligi ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Simba. Mpaka sasa Mgunda ni Kocha Mkuu wa muda na msako wa kocha mpya unaendelea. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Simba ameweka wazi kuwa mwendo wa Mgunda sio mbaya kwa kuwa amepata mazuri. “Mwendo wake sio mbaya, mechi tatu na zote kashinda, lakini mkataa w...

VIDEO: YANGA WAAMBIWA WAJIFUNZE KWA WATANI ZAO

Image
  MWANDISHI mkongwe wa masuala ya michezo Afrika Mashariki na Kati, Saleh Jembe ameweka wazi kuwa kimataifa sio kwepesi ni lazima kwa Yanga kujifunza ili kupata matokeo kwenye mechi zote watakazocheza

KOCHA TAIFA STARS ABEBA MATUMAINI KIMATAIFA

Image
  HONOUR Janza, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wtacheza kwa kujiamini kwenye mechi za kirafiki za kimataifa zilizo kwenye Kalenda ya FIFA ili kupata matokeo. Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uganda na Libya ambazo zitachezwa nchini Libya na kikosi hicho kilikwea pipa jana, Septemba 20 kuelekea Libya. Katika msafara huo miongoni mwa nyota ambao walikuwa katika kikosi hicho ni pamoja na Said Ndemla kiungo anayekipiga Singida Big Stars ambaye aliongezwa kwenye orodha ya wachezaji wa Stars, Himi Mao,Dickson Job,Aishi Manula ni miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye msafara huo.  Kocha huyo amesema:”Tunaamini mechi hizi za kimataifa za kirafiki zitazidi kutuimarisha na tutafanya kazi kubwa kwa kucheza kwa kujiamini ili kupata ushindi, wachezaji wapo tayari na tunaamini tutafanya vizuri,” . Stars imewasili salama nchini Libya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mechi hizo mbili. Tanzania itaanza kucheza na timu ya Taifa ya ...

SSEMWOGERERE KOCHA MPYA PAMBA FC

Image
  NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda, George Ssemwogerere ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Pamba ya Mwanza akichukua nafasi ya Mkenya, Yussuf Chipo aliyehamia Coastal Union ya Tanga. Pamba, mabingwa wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapambana kurejea Ligi Kuu kutoka Championship iliyoanza mwishoni mwa wiki wakipata ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Ken Gold ya Mbeya. Mechi hiyo ya kwanza timu ilikuwa chini ya kocha mwingine mzoefu nchini, Steven Matata aliyekuwa Msaidizi wa Chipo wakati wa maandalizi ya msimu na mechi ijayo Jumamosi dhidi ya Mbeya Kwanza ndiyo Ssemwogerere ataanza kazi.

KMC YAICHAPA IHEFU SC 2-1 UWANJA WA UHURU

Image
  WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mabao ya KMC yamefungwa na Matheo Anthony dakika ya tatu na Nzigamasabo Steve dakika ya 77, wakati la Ihefu SC limefungwa na Raphael Daudi dakika y 34. KMC inafikisha pointi tano baada ya ushindi huo ikisogea nafasi ya nane, wakati Ihefu inaendelea kuwa timu pekee ambayo haijavuna pointi hadi sasa kufuatia wote kucheza mechi nne.

ALLY MAYAY TEMBELE MKURUGENZI MPYA WA MICHEZO

Image
  ALIYEWAHI kuwa Nahodha wa timu ya taifa na klabu ya Yanga, Ally Mayayi Tembele ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo akichukua nafasi ya Yusuph Singo.

NABI AFICHUA SABABU YA KUTOFUNGWA DK 3,600

Image
  NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amefichua kuwa kutopoteza kwenye mechi za ligi kwa muda mrefu kunatokana na jitihada za wachezaji kusaka ushindi. Ni mechi 40 za ligi Nabi kaongoza bila kuonja ladha ya kupoteza mchezo ikiwa ni dakika 3,600 zimeyeyuka.  Aprili 25,2021 ilikuwa ni mara ya mwisho Yanga kufungwa ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Nabi amesema kuwa sio kitu rahisi kucheza mechi nyingi bila kufungwa na inahitaji juhudi zaidi kwa wachezaji kupata matokeo. “Unaona kwamba msimu huu ligi ni ngumu na kilamechi tunatambua kwamba itakuwa na ushindani mkubwa, sio rahisi kushinda mechi zote na ili tusifungwe ni lazima tuongeza juhudi. “Wachezaji nimewaambia kwamba kazi yetu moja ni kutafuta ushindi kwenye mechi zote bila kujali tunacheza na timu ipi, mfano mchezo wetu dhidi ya Azam kabla hatujacheza nao nilijua utakuwa mgumu. “Kuwaangalia wapinzani wakiwa wanacheza haina maana kwamba inaweza kukupa matokeo unayotaka kwenye mechi ...

RATIBA ZA MECHI KUBADILISHWA ENGLAND

Image
  RATIBA za mechi za Ligi Kuu England zinaweza kubadilika kutokana na kutangulia mbele za haki kwa Queens Elizabeth.. Miongoni mwa michezo ambayo ilipaswa kuchezwa Ijumaa ya Ligi Kuu England ambao ni Burnley v Norwich, Tnanmere v Stocport imeweza kughairishwa kutokana na kutangulia mbele za haki kwa Queen Elizabeth. Hii yote inafanywa kutokana na heshima ya kiongozi huyo na majadiliano yalifanyika kwa  pande zote huku Serikali pia kwa sas ikifanya majadiliano kuhusu ratiba zingine. Kwenye mechi ya Manchester United kulikuwa na utulivu wa dakika moja kutokana na msiba huo.

NAMUNGO FC WAREJEA NYUMBANI,UWANJA WA KISASA BALAA

Image
  UWANJA wa Majaliwa sasa utatumika kwa mechi za nyumbani kwa Klabu ya Namungo baada ya kufanyiwa ambayo yalichukua muda mrefu. Wakati wa maboresho hayo Namungo FC ilikuwa inatumia Uwanja wa Ilulu, Lindi na ulipofungiwa ili ufanyiwe maboresho walikuwa wanatumia Uwanja wa Mkapa na Uhuru kwa mechi za nyumbani. Mazoezi yao ya kwanza ilikuwa ni Septemba 7,2022 na mashabiki wengi walijitokeza kushuhudia timu hiyo ikifanya mazoezi kwenye uwanja wao ambao kwa sasa una muonekano bora na wa kisasa zaidi. Kinara wa utupiaji mabao ndani ya Namungo, Relliats Lusajo amesema kuwa kurejea kwao ni furaha na wataendelea kupambana kufanya vizuri. “Tulikuwa nje kwa muda mrefu na tulikuwa tukitumia Uwanja wa Ilulu sasa tumerudi Uwanja wa Majaliwa hili ni jambo la kubwa kwetu. “Haina maana kwamba Uwanja wa Ilulu haikuwa nyumbani hapana kuna kitu kinaongezeka kurejea kwenye uwanja ambao tulikuwa tukiutumia kwa muda mrefu na tunaamini kwamba mashabiki watazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Lusajo.

VIDEO:WAPINZANI WA YANGA, ZALAN KUWASILI LEO

Image
  WAPINZANI wa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Zalan FC wanatarajiwa kuwasili leo Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 10,2022 ambapo Zalan wao watakuwa wenyeji wa mchezo huo

VIDEO:JEMBE AZUNGUMZIA SAKATA LA KISINDA NA MGUNDA KUINOA SIMBA

Image
  MWANDISHI mkongwe kwenye masuala ya habari za michezo, Saleh Ally Jembe amezungumzia suala la Tuisila Kisinda pamoja na Juma Mgunda kujiunga na Simba

SAUTI:MPANGO WA BOCCO KUSEPA SIMBA UPO HIVI

Image
  INAELEZWA kuwa nyota wa Simba na nahodha wa kikosi hicho, John Bocco mpango wake ulikuwa ni kupata changamoto mpya