YANGA ‘OUT’ LIGI YA MABINGWA, YAANGUKIA SHIRIKISHO

 


TIMU ya Yanga imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Al Hilal katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora leo Uwanja wa Al Hilal mjini Omdurman nchini Sudan.
Bao lililoizamisha Yanga limefungwa na Mohamed Abdelhaman dakika tatu ya mchezo huo na kwa matokeo hayo Hilal wanakwenda Hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Dar es Salaam.
Yanga wao watakwenda kujaribu bahati yao kwa kuwania kucheza Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Comments

Popular posts from this blog

HAJI MANARA AMPONGEZA ALLY KAMWE KUTEULIWA YANGA

AZAM FC YASHINDA 2-0 CHAMAZI, LAKINI YATOLEWA

WAWAKILISHI WA KIMATAIFA YANGA KUREJEA DAR