Posts

Showing posts from October, 2022

YANGA NGUVU ZOTE KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
  UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kwa sasa akili zote zinaelekezwa kwenye mechi za Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushindwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi iliondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa ilikubali sare ya bao 1-1 na ule wa pili ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0. Rais wa Yanga, Hers Said amesema kuwa hakuna wa kumlaumu kwa kushindwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo wanajipanga Kombe la Shirikisho. “Tumeshindwa kupata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya Al Hilal hatuna wa kumlaumu kwa sasa hivyo kikubwa ni kujipanga kwa ajili Kombe la Shirikisho ambalo nalo ni mechi za kimataifa. “Sisi kauli mbiu yetu kubwa ni daima mbele nyuma mwiko hivyo tunaendelea mbele na yale makosa ambayo yametokea nina amini benchi la ufundi litayafanyia kazi ili kuwa imara kwa wakati ujao,” . Miongoni mwa nyota amb...

WAWAKILISHI WA KIMATAIFA YANGA KUREJEA DAR

Image
  BAADA ya kupoteza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal, kikosi cha Yanga leo kimeanza safari ya kurejea Tanzania. Msafara huo ambao uliongozana na viongozi utapitia Addis Ababa Ethiopia. Bado Yanga inabaki kwenye anga za kimataifa kwa kuwa imeangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrka. Inafanya zibaki timu mbili Tanzania ambazo zinapeperusha bendera ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Simba. Azam FC na Kipanga wao jitihada zao ziligota mwisho baada ya kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zao ambazo walicheza. Azam licha ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Al Akhadar ya Libya imeondolewa kwa jumla ya mabao3-2 kwa kuwa mchezo wa ugenini ilipoteza huku Kipanga wenyewe wakiondolewa kwa jumla ya mabao 7-0 dhidi ya Club Aficain.

SIMBA SC YATINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
  WENYEJI, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Primiero de Agosto ya Angola katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la Simba SC leo limefungwa na mshambuliaji wake Mzambia, Mosea Phiri dakika ya 33 na sasa Wekundu wa Msimbazi wanakwenda Hatua ya Makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kuwafunga 3-1 Agosto kwao, Luanda wiki iliyopita.

AZAM FC YASHINDA 2-0 CHAMAZI, LAKINI YATOLEWA

Image
  WENYEJI, Azam FC wametupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Akhdar ya Libya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Idris Mbombo dakika ya 28 na Ededen Essien aliyejifunga dakika ya 59 na kwa matokeo hayo Al Akhdar inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mechi ya kwanza.

YANGA ‘OUT’ LIGI YA MABINGWA, YAANGUKIA SHIRIKISHO

Image
  TIMU ya Yanga imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Al Hilal katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora leo Uwanja wa Al Hilal mjini Omdurman nchini Sudan. Bao lililoizamisha Yanga limefungwa na Mohamed Abdelhaman dakika tatu ya mchezo huo na kwa matokeo hayo Hilal wanakwenda Hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Dar es Salaam. Yanga wao watakwenda kujaribu bahati yao kwa kuwania kucheza Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.